MBOMBO AREJESHA MATUMAINI AZAM.

Na: Stella Kessy, DAR ES SALAAM.

KLABU ya Azam leo imejinyakulia pointi 3 mbele ya Namungo kwa bao 1-0 katika michuano ya ligi kuu Tanzania bara uliopigwa katika dimba la Chamanzi.

Mtanange huo  uliokuwa na ushindani kwa kila timu mpaka kumalizika  kipindi cha kwanza hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake.

Katika dakika ya 89 mshambuliaji Idriss Mbombo aliipatia timu yake bao la pekee ambalo limedumu dakika zote za mchezo.

Kwa sasa Azam inakuwa na jumla ya point nne ikitoka sare  dhidi ya Coastal nakufungwa na Polisi Tanzania  huku ikiibuka na ushindi leo dhidi ya Namungo.

Hata hivyo kikosi cha  Azam kesho kinaondoka kuelekea Misri katika mchezo wao wa marudio dhidi ya Pyramids katika michuano ya kombe la shirikisho.


Post a Comment

0 Comments